Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanachama wa UM wanahitaji ushujaa: Deiss

Wanachama wa UM wanahitaji ushujaa: Deiss

Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Joseph Deiss amesema wanachama wa Umoja wa Mataifa wanahitaji kuonyesha ujasiri ili kuvuka viunzi vya kufikia amani duniani.

Deiss ameyasema hayo na mengine katika kuhitimisha mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa. Mjadala huo wa kila mwaka unaowajumisha wakuu wan chi na wawakilishi wa serikali ulikuwa unafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York.

Mjada huo umetoa wito kwa wanachama wote kuweka kando mzunguko wa masuala ya uchaguzi na kukumbatia maslahi ya taifa. Jason Nyakundi anaarifu.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)