Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kesho Oktoba mosi ni siku ya wazee duniani

Kesho Oktoba mosi ni siku ya wazee duniani

Kesho Oktoba mosi ni siku ya kimataifa ya wazee siku ambayo imetengwa rasmi na baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Desemba 14 mwaka 1990 baraza hilo lilipitisha azimio namba 45/106 ikiwa ni kutokana na mikakati mingine iliyotangulia kama mpango wa Vieena kwa ajili ya wazee uliopitishwa 1882 na azimio namba 46/91 la sheria kuhusu wazee zilizopitishwa na baraza kuu la umoja wa Mataifa mwaka 1991.

Kwa mujibu wa baraza la kuu la Umoja wa Mataifa siku hiyo imetengwa maalumu kwa ajili ya kukabiliana na changamoto zinazowakabikli watu wengi ambao wanazeeka katika karne hii ya 21, kuchagiza mchango wa maendeleo katika jamii kwa watu wa rika zote na kutoa fursa kwa wazee kuchangia katika masuala ya jamii.