Ban na Kagame wajadili masuala mbalimbali

27 Septemba 2010

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon jana Jumapili amefanya mkutano maalumu na Rais Paul Kagame wa Rwanda kando na mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Katika mkutano wao wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo afya na mama na mtoto. Ban amemshukuru Rais Kagame na nchi yake kwa jukumu lao la kuhakikisha hatua imepigwa katika kuelekea kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia. Ban pia amesema ameridhika baada ya kutambua kwamba Rwanda itaendelea kujihusisha na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani na hasa kwenye jimbo la Darfur Sudan.

Masuala mengine walijadili ni ripoti kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itakayotolewa Oktoba mosi, ambayo inaelezea vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo kati ya mwaka 1993 na 2003 ambapo maelfu ya watu waliuawa.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter