UM na AU wazindua jopo kushughulikia amani na usalama

UM na AU wazindua jopo kushughulikia amani na usalama

Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika AU kwa pamoja wamezindua jopo litakaloshughulikia masuala ya amani na usalama.

Jopo hilo litashughulikia amani na usalama wakati mashirika hayo mawili yakiwa katika juhudi za kuzuia kutokea na kuendelea kwa mizozo na kuhakikisha amani inatawala kote barani Afrika. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Jopo hilo lililozinduliwa mjinji New York na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon pamoja na mwenyekiti wa AU Jean Ping litakuwa likikutana mara mbili kila mwaka kutathimini na kupanga mikakati yake. Ban na Ping wamesema kuwa wangependa kuwe na ushirikiano zaidi kati ya Umoja wa Matifa na Muungano wa Afrika zaidi na ule uliopo kwenye harakati zao nchini Sudan, Guinea na Somalia.

Kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na kile cha Muungano wa afrika kinachofahamika kama UNAMID kimekuwa kwenye harakati za kulinda amani kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan tangu mwaka 2008 huku pia Umoja wa mataifa ukitoa usaidizi kwa kikosi cha AMISON kinacholinda amani nchini Somalia.