Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kura ya turufu iondolewe kwenye baraza la usalama:Iran

Kura ya turufu iondolewe kwenye baraza la usalama:Iran

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad ametoa wito wa kutaka kuondolewa kwa kura ya turufu waliyo nayo wanachama watano wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Matifa.

Ahmadinejad amesema kuwa Umoja wa Matifa unastahili kufanyiwa mabadiliko ili mataifa yote yaweze kushiriki vilivyo kwenye uongozi wa dunia. Ameongeza kuwa kura ya turufu inayapa wanachama hao mamlaka zaidi akisema hakutakuwa na haki wakati wa wanachama wote wa baraza hilo wanapoegemea upande mmoja.

Maamuzi ya masuala muhimu ya baraza la usalama la Umoja wa Matifa huwa yanahitaji kura ya turufu kutoka kwa wanachama tisa kati ya kumi na tano wa baraza hilo na kura zote za wanachama wa kudumu wakiwemo Marekani , Urusi , China , Uingereza na Ufaransa.