Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umezitaka nchi kupiga hatua katika mazungumzo ya kimataifa ya upokonyaji silaha

UM umezitaka nchi kupiga hatua katika mazungumzo ya kimataifa ya upokonyaji silaha

Mjadala katika baraza kuu la Umoja wa Mataifa unaendelea huku masuala mbalimbali yakijadiliwa. Leo maafisa wa Umoja wa Mataifa wamezitaka nchi kupiga hatua katika upokonyaji silaha wa kimataifa na pia kuongeza juhudi kutokomeza silaha za maangamizi.

kizungumza katika mkutano huo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema wote tunaamini kwamba njia za upokonyaji silaha lazima zitoe matunda na haraka, amesema ni utashi wa kisiasa pekee wa wanachama wa Umoja wa Mataifa utakaofanikisha hilo. Ameongeza kuwa ni muhimu kutokomeza silaha hizo kwa sababu nyingi.

(SAUTI BAN KI-MOON)

Ban hata hivyo amekumbushia hatua zilizopigwa hivi karibuni katika juhudi za upokonyaji silaha ikiwa ni pamoja na mkataba mpya wa kudhubiti na kupunguza umiliki wa silaha START ambapo Matrekani na Urusi walitia sahihi.