Ni miaka mitano imesalia kutimiza malengo ya milenia Burundi imefika wapi?

Ni miaka mitano imesalia kutimiza malengo ya milenia Burundi imefika wapi?

Wakati viongozi wa dunia wanaendelea na mkutano wa kutathimini hatua zilizopigwa kufikia malengo ya amaendeleo ya milenia kuna baadhi ya nchi bado zinasua sua hususani nchi masikini za bara la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.

Burundi ambayo ni hivi majuzi tuu imefanya uchaguzi wa pili wa kidemokrasia baada ya muongo wa machafuko inasema imejitahidi katika baadhi ya mambo lakini bado kuna mengine inajikongoja hasa kutokana na mchafuko ya muda mrefu nchini humo.

Lengo la kwanza la milenia ni kutokomeza umasikini na njaa je wamepiga hatua kiasi gani katika hili? Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa mjini Bujumbura Ramadhani Kibuga anatathimini katika makala hii.