Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waliopoteza makazi Zimbabwe wasitirika:IOM

Waliopoteza makazi Zimbabwe wasitirika:IOM

Zaidi ya familia 340 zilizopoteza makazi kufuatia ghasia kwenye eneo la Chipinge mashariki mwa Zimbabawe mwaka uliopita kwa sasa zinapata usaidizi wa kupata makao mapya.

Zoezi la kuzihamisha familia hizo ambazo zimekuwa zikiishi kwenye makao ya muda tangu mwaka 2009 linaendeshwa la shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na serikali ya Zimbabwe.Kati ya shughuli zinazotekelewa na IOM ni pamoja na kuzisafirisha famia hizo kwenda kijiji tofauti, kuzijengea makao, kuwahakikisha wana maji na vyoo pamoja na madarasa ya kusomea.

IOM pila linahakikisha kuwa familia hizo zimepata hati halali za kumiliki ardhi. Mabadiliko kuhusu umiliki wa ardhi yaliyoanza mwaka 2000 yaliyoambatana na ghasia zilizofuatia uchaguzi wa mwaka 2008 yalisababisha kutokea kwa mizozo ya ardhi miongoni mwa familia nyingi nchini humo.

Shughuli hii ya kuzipa makao mapya familia zilizopoteza makwao ni ishara tosha jinsi ushirikiano kati aya seriklia, jamii na mashirikia ya kutoa huduma za kibinadamu wanaweza kushirikiana kupata suluhu kwa wakimbizi wa ndani.