Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa aunga mkono juhudi za kupatikana kwa suluhu la kudumu kwa wakimbizi wa ndani nchini Georgia

16 Septemba 2010

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masaula ya wakimbizi wa ndani amesema kuwa kupatikana kwa suluhu la kudumu kwa wakimbizi wa ndani nchini Georgia ni suala linalostahili kupewa umuhimu mkubwa.

Akikamilisha ziara ya siku nne nchini Georgia Walter Kaelin ambaye ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia haki za wakimbizi wa ndani amesema kuwa hata kama serikali ya Georgia imepiga hatua kuwashughulikia wakimbizi wa ndani bado inahitaji kufanya juhudi zaidi. Akiguzia suala la kufungwa kwa kambi za wakimbizi Kaelin ametaka kuwepo kwa mpangilio wa jinsi ya kufungwa kwa vituo hivyo ili kuhakikisha kuwa shughuli ya kuondolewa kwa wakimbizi kwenye vituo vyao inazingatia mipangilio ya kimataifa. Kaelin ameongeza kuwa wakimbizi kama hao wanastahili kutafutiwa makao au njia zingine za kuendeleza maisha mapema, kabla ya kufungwa kwa vituo wanamoishi bila ya wao kupoteza tegemeo lao maishani pamoja na huduma zingine zikiwemo za elimu na afya.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter