Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yapongeza au kuridihia mkataba wa wakimbizi wa ndani

UNHCR yapongeza au kuridihia mkataba wa wakimbizi wa ndani

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeridhishwa na hatua ya Umoja wa Afrika AU kuridhia mkataba wa kwanza kuwalinda wakimbizi wa ndani barani Afrika.

UNHCR inasema kwamba mkataba huo ulioridhiwa nchini Uganda wa kuwalinda na kusaidia wakimbizi wa ndani Afrika katika kipindi cha miezi mine tangu kupitishwa ni hatua kubwa na muhimu sana.

Mkataba huo uliridhiwa katika mkutano wa kwanza maalumu wa Umoja wa Afrika uliofanyika mjini Kampaka mwezi Octoba mwaka 2009 ambao ulikuwa ukijadili masuala ya wakimbizi, watu wanaorejea makwao na wakimbizi wa ndani.

UNHCR imebaini kwamba nchi 25 au karibu nusu ya nchi zote wanachama wa Umoja wa Afrika hivi sasa wametia saini mkataba huo, ambao ni wa kwanza wa kisheria unaotetea maslahi ya wakimbizi wa ndani katika bara hilo.

Sahihi 15 zingine zinahitajika ili mkataba huo uanze kutekelezwa. UNHCR inazichagiza nchi nyingine wanachama wa AU kufuta mfano wa Uganda na kuridhia mkataba hio, ili uanze kufanya kazi mwishoni mwa mwaka huu wa 2010 kama waliyotaka viongozi wa Afrika kwenye mkutano huo.

UNHCR inakadiria kuwa kuanzia mwanzoni mwa mwaka jana kulikuwa na wakimbizi wa ndani zaidi ya milioni kumi na mioja na nusu, waliokimbia migogoro Afrika, na idadi hiyo ni karibu nusu ya wakimbizi wote wa ndani duniani.