Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa kimeanza New York

Kikao cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa kimeanza New York

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linaanza mkutano wake wa 65 hii leo kwenye makao makuu huku suala la maendeleo, mazingira na mageuzi katika Umoja huo wa Mataifa, zikiwa ni mada kuu za majadiliano.

Rais wa Baraza hilo Joseph Deiss amesema kuwa viongozi wa nchi wanachama watazingatia kutilia mkazo kuhusu umuhimu wa kuwa na mazingira endelevu kwa shabaya ya kuhimiza maendeleo hasa wakati huu ambapo mkazo unawekwa kwenye kuyafikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Rais huyo ambaye ni raia wa Uswis ameeleza kuwa kunamatumaini makubwa ya kufikiwa kwa malengo hayo ya mellenia licha ya kuwepo kwa vikwazo vya hapa na pale ikiwemo hali ya mkwamo wa uchumi wa dunia iliyojitokeza katika siku za hivi karibuni.

Bwana Deiss ameelezea matumaini yake kuwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akisema linaweza kutoa mchango mkubwa katika masuala ya ulimwengu.