Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unilever imekusanya fedha kusaidia kuwalisha wanafunzi Kenya

Unilever imekusanya fedha kusaidia kuwalisha wanafunzi Kenya

Shirika moja la kijerumani Unilever limekusanya zaidi ya Euros 100,000 kwa ajili ya kugharimia mahitaji ya chakula kwa wananfunzi nchini Kenya.

Wafanyakazi wa shirika hilo wakiwa wamevalia fulani zenye ujumbe usemayo " tuungeni mkono" walijisambaza kwenye maduka makubwa yaliyoko Mjini Hamburg na kuanzakuuza bidhaa aina siagi kwa shabaya ya kuchangisha fedha ya kugharimia watoto wa shule nchini Kenya.

Baadhi ya wafanyakazi hao walikuwa wameshika vipeperushi vilivyokuwa na ujumbe toka kwa shirika WFP,walisema kuwa wamedhamiria kuzisaidia familia maskini ambazo wakati mwingine zinashindwa kugharimia mahitaji yao muhimu ikiwemo chakula.

Kenya ni miongoni mwa mataifa yanayosaidiwa huduma ya chakula toka kwa WFP inayoshirikiana na Uniliver. Zaidi ya watoto 700,000 wamekuwa wakipatiwa msaada huo wa chakula.