Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umeanzisha kampeni kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia nchini Haiti

UM umeanzisha kampeni kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia nchini Haiti

Umoja wa Mataifa umeanzisha operesheni maalumu ya kukabiliana na vitendo vya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia nchini Haiti, ambako mamilioni ya watu wameendelea kukosa makazi kufuatia tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo mwezi January mwaka huuu.

Bado kuna idadi kubwa ya watu wanaendelea kuishi kwenye mahema kutokana na nyumba zao kuharibiwa vibaya na tetemeko hilo. Askari polisi pamoja na vikosi vya ulinzi vinavyofanya kazi chini ya kivuli cha kikosi maalumu cha umoja wa Mataifa MINUSTAH wameanza kupatiwa mafunzo ya kukabiliana na vitendo hivyo na wakati huo kuwa tayari kutoa huduma za matibabu kwa waathiriwa.

Mkuu wa kikosi hicho cha MINUSTAH Edmond Mulet amekiambia kikao cha Baraza la usalama kuwa wanawake na watoto wako hatarini zaidi kukubwa na vitendo vya ubakaji pamoja na unyanyasaji wa kijinsia. Amesema kuwa kwa kutoa mafunzo kwa vikosi hivyo hali inaweza kudhibitiwa.