UM waonya juu ya watu kuhamishwa kwa nguvu Kazakhstan

UM waonya juu ya watu kuhamishwa kwa nguvu Kazakhstan

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya makazi Raquel Rolnik ametoa tahadhari kuhusu watu kufukuzwa kwa nguvu kwenye makazi yao nchini Kazakhstan.

Hatua hiyo inafanyika ili kutoa fursa kwa miradi ya maendeleo yenye lengo la kuchangia ukuaji wa uchumi na jamii.

Bi Rolnik amesema watu kuondolewa kwa lazima kutoka makazi yao kunastahili kufanyika kwa kuzingatia sheria za kimataifa zinazolinda haki za binadamu. Maelezo zaidi na Jason Nyakundi

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)