Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mauwaji ya raia wanne wa Israel huko ukanda wa Magharibi.

Ban alaani mauwaji ya raia wanne wa Israel huko ukanda wa Magharibi.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mauwaji ya raia wanne wa Israel katika mji wa Hebron ukanda wa Magharibi siku ya Jumanne, siku kadhaa kabla ya kuanza kwa mazungumzo ya ana kwa ana kati ya viongozi wa Israel na Palestina mjini Washington.

Waisraeli hao wanne wanaume wawili na wanawake wawili, moja akiripotiwa ni mjamzito, walikua wanasafiri ndani ya gari karibu na Hebron waliposhambulia kwa bunduki na kuuwawa. Katika taarifa yake Bw Ban alitoa mkono wa rambi rambi kwa familia za waathiriwa na kutoa wito kwa wahusika wa shambulio hilo wafikishwe mara moja mbele ya sheria.

Taarifa inaeleza kwamba ni lazima kuchukulia shambulio hilo kua ni jaribiyo la kutaka kuhujumu majadiliano kati ya Israel na Palestina yanayoanza kesho. Ikiongezea kwamba majadiliano ndio njia pekee kwa pande zote kutanzua masuala yote ya awamu ya mwisho. Nae Katibu Mkuu ametoa wito kwa pande zote mbili kuonesha uwongozi, ushujaa na uwajibikaji katika kutekeleza ndoto ya wananchi wa pande zote mbili.

Serikali ya Marekani imeandaa mazungumzo ya ana kwa ana kuanzia tarehe mbili Septembe kati ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na rais wa utawala wa Palestina Mahamoud Abass.