Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM anatoa wito wa kukomesha hali kutohukumiwa wahalifu huko DRC

Mwakilishi wa UM anatoa wito wa kukomesha hali kutohukumiwa wahalifu huko DRC

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kwa ajili ya unyanyasaji wa ngono katika vita, amesema mashambulio ya hivi karibuni ya ubakaji wa raia na waasi huko mashariki ya Jamhuri ya Kongo yanasisitiza haja ya kukomesha hali ya kutohukumiwa wahusika wa uhalifu kama huo.

Akizungumza na waandishi habari mjini New York Bi Margot Wallstrom alisisitiza kwamba ni lazima kwa serikali ya DRC kubadili sera zake za kupambana na unyanyasaji wa ngono na kua na sera zenye uwajibikaji wa dhahir na sambaba kwa watenda maovu hayo. Kiasi ya raia 154 walibakwa katika vijiji 13 vilivyo kando ya barabara muhimum yenye urefu wa km 21 katika wilaya ya Banamukira jimbo la Kivu kaskazini kati ya Julai 30 na Agosti 2. Washambuloizi walifunga njia na kuwazuia wanavijiji kuwasiliana na watu wa nje.

Bi Wallastrom aliwakumbusha viongozi wa kisiasa wa kundi la waasi la FDLR na Mai Mai kwamba ubakaji unaodaiwa ulifanywa na wapiganaji wao ni uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu"

(SAUTI YA WALLSTROM)

Bi Wallastrom alisema shambulio la ubakaji wa mara kwa mara huwa limepangwa na hivyo linaweza kuzuiliwa na ubakaji wa Kivu ya Kaskazini uasisitiza juu ya jinsi amani na utulivu hauwezi kudumishwa huko DRC hadi pale usalama wa wamawake unahakikishwa.