Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatilia shaka namna ya wanawake wanavyoongezeka kwenye uvutaji wa sigara

WHO yatilia shaka namna ya wanawake wanavyoongezeka kwenye uvutaji wa sigara

Shirika la afya duniani WHO limeonya kwamba wanawake duniani kote wanakabiliwa na tishio la uvutaji wa sigara na hivyo kukaribisha maradhi yakiwemo kansa.

Katika ripoti yake iliyoangazia hali ya uvutaji wa sigara WHO imesema kuwa, kundi la wanawawake na wanaochipukia kwenye uvutaji wa sigara imeendelea kuongezeka na sasa imefikia asilimia 20 ya wavutaji sigara wanaosadikika kuzidi bilioni 1.

Pamoja na kusisitiza kwamba uvutaji wa sigara husababisha maradhi ya kansa kwa wavutaji wa kike na kiume, lakini wanawake wapo hatarini zaidi kwani wanakabiliwa na maradhi mengi ikiwemo tatizo la kutopumua vizuri, magonjwa ya moyo na matatizo mengine ya kiafya.

WHO imesema kuwa matangazo mengi yanayohamasisha sigara kwa hivi sasa yamekuwa yakiwalenga zaidi kina dada na hivyo kuwatumbukiza kwenye mtego wa utumiaji wa tumbaku.

==