Skip to main content

Tume ya UM ya uchunguzi wa flotilla yatoa taarifa

Tume ya UM ya uchunguzi wa flotilla yatoa taarifa

Ripoti ya pili ya ufuatiliaji wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi dhidi ya shambulio la flotilla Gaza imetolewa.

Ripoti hiyo inajumuisha taarifa zilizokusanywa hadi sasa kutoka pande zote, yaani Israel na Palestina katika juhudi za kupata ukweli kuhusu madai ya kukiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu wakati wa shambulizi la flotilla. Ripoti hiyo pia ina maelezo mafupi yaliyokusanywa na serikali ya Switzerland kuhusu kuanzishwa kwa mkutano baiana ya pande hizo mbili.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amerejea kusema anaamini kwamba sheria na haki za kimataifa za binadamu lazima ziheshimiwe kikamilifu. Amesema ni matumaini yake kwamba azimio 64/254 litakuwa limetekelezwa kuchagiza uchunguzi huru wa serikali ya Israel na Palestina ambao ni huru na unaozingatia viwango vya kimataifa.