Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP inapanua wigo wa kazi kwa fedha nchini Iraq

WFP inapanua wigo wa kazi kwa fedha nchini Iraq

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linapanua wigo wake wa mpango wa fedha kwa kazi nchini Iraq kwa kuwalenga wasio na ajira katika maeneo yaliyoathirika zaidi na ghasia na ukosefu wa usalama.

Lengo la mradi huo ni kuwafikiwa watu 11,000 na kuwasaidia kukidhi mahitaji yao ya kila siku ya chakula. Mpango huo unawapa wasio na kazi ajira ya muda mfupi katika miradi ya kilimo ili kuwapa hakikisho la muda mrifu la kutokabiliwa na upungufu wa chakula.

Baadhi ya maeneo yatakayofaidika na mradi huo ni Diyala na Baghdad ambako watu wengi wamerejea kutoka ng'ambo au kutoka katika maeneo mengine ya Iraq na kukuta nyumba na mali zao zimeporwa na pia wamepoteza kazi.