Maelfu ya wakimbizi wa ndani warejea Kivu DR Congo:UNHCR
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema maelfu ya wakimbizi wa ndani wanaendelea kurejea nyumbani Kivu ya Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .
Shirika hilo linasema kurejea nyumbani kwa wakimbizi hao ni nyota njema katika nchi ambayo bado imeghubikwa na machafuko na sehemu zingine watu wanaendelea kuzihama nyumba zao kukimbia vita.
Hata hivyo UNHCR inasema pamoja na hatua hiyo kubwa wakimbizi hao wanaorejea wanakabiliwa na changamoto kubwa mbele yao.
Kamishina mkuu wa shirika lwa wakimbizi duniani Antonio Guterres anasema ni muhimu kuendelea kuwasaidia wakimbizi hao ili kujenga upya maisha yao.
Vita Kivu ya Kaskazini vilichacha mwaka 1996 baada ya wapiganaji wa Kihutu kutoka nchi jirani ya Rwanda wa FDLR walipovamia eneo hilo na kuanza kupambana na jeshi la serikali ya Congo.