Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuzindua muongo wa vita dhidi ya jangwa Agost 16

UM kuzindua muongo wa vita dhidi ya jangwa Agost 16

Umoja wa Mataifa hapo Jumatatu Agosti 16 utazindia muongo wa vita dhidi ya ukame na jangwa. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingitra UNEP hafla maalumu ya uzinduzi huo itafanyika mjini Fortaleza nchini Brazili.

UNEP inasema matatizo ya jangwa duaniani yanaongezeka kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni ukilinganisha na miongo kadhaa iliyopita na linasema jinsi janga linavyoongezeka linaambatana na athari nyingine kwa maisha ya binadamu na wanyama.

Baadhi ya athari hizo zimetajwa kuwa upungufu wa chakula na makazi. Na bara la Afrika limetajwa kuwa ni moja ya mabara yaliyo katika hatari kubwa huku watu wake takribani milioni 22 wakiishi katika ardhi iliyo na tisho la kugeuka jangwa.