Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushelisheli yaongeza idadi ya wanachama wa mahakama ya ICC

Ushelisheli yaongeza idadi ya wanachama wa mahakama ya ICC

Visiwa vya Ushelisheli vilivyo katika bahari ya Hindi vimekuwa nchi ya hivi karibuni kuwa mwanachama wa makahama ya kimakataifa kuhusu uhalifu ICC ambayo imepewa jukumu la kuwashtaki na kuwahukumu watu wanaokabiliwa na vitendo vya mauaji ya halaiki ,uhalifu wa kivita pamoja na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Hii inamaanisha kuwa ushelisheli itakuwa mwanachama kamili wa mahakama hiyo kuanzia tarehe mosi mwezi Novemba mwaka huu kulingana na habari iliyotolewa na mahakama hiyo yenye makao yake makuu mjini Hague nchini uholanzi.

Mahakama ya ICC iliundwa mwaka 2002 baada ya nchi 60 kuwa wanachama mwaka huo na sasa kujiunga kwa ushelisheli kunafikisha idadi ya wanachamacha wa mahakama hiyo kufikia mataifa 112. Kwa sasa mahama ya ICC inaendesha uchunguzi katika nchi tano zikiwemo Uganda , Jamhuri ya kidemokrasi ya kongo, jimbo la Darfur nchini Sudan , Jamhuri ya afrika ya kati na Kenya.