Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa usalama waweza kutishia uchaguzi Aghanistan

Ukosefu wa usalama waweza kutishia uchaguzi Aghanistan

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini Afghanistan Staffan de Mistura amesema nchi hiyo sasa imejikita katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Wolesi Jirga ambao umesaliza siku 37 tuu kabla ya kufanyika.

De Mistura amesema katika tathimini yake ameona kuna wagombea wengi waliojitokeza na wanafanya kampeni na ametiwa moyo zaidi na idadi ya wagombea wanawake. Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa unasimama na jukumu lake la kuisaidia Afghanistan kuwa na uchaguzi mzuri wanaostahili. Tume huru ya uchaguzi nchini humo IEC inaendelea kutimiza wajibu wake kama ratiba ilivyopangwa, na karatasi muhimu za kupigia kura zimeshawasili nchini humo tangu wiki jana.

Pamoja na mafanikio hayo Bwana De Mistura ametaja pia changamoto katika uchaguzi huo na kubwa ni usalama ambao amesema unaweza kutia dosari uchaguzi mzima. Amesema wameshuhudia vitisho hasa kwa wagombea wanawake, mauaji ya wagombea watatu na ghasia zingine dhidi ya wagombea. Amesema vitendo hivyo havikubaliki na ametoa wito kwa vikosi vya ulinzi na usalama vya Afghanistan kuwa na tahadhari ya hali ya juu katika miezi michache ijayo.