Wanajeshi wanne wa kulinda amani wa UNAMID wafariki dunia katika ajali

2 Agosti 2010

Taarifa kutoka Sudan zinasema wanajeshi wane wa kulinda amani wa vikosi vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID wamefariki dunia katika ajali.

Kwa mujibu wa UNAMID wanajeshi hao ni kutoka Sierra Leone na walikufa jana jioni baada ya gari lao kugongana katika ajali ya barabarani kwenye eneo la Nyala Kusini mwa Darfur.

UNAMID ni moja ya jeshi kubwa kabisa la kulinda amani duniani na liko kwenye jimbo la Darfur lililoghubikwa na machafuko, ili kuhakikisha usalama kwa maelfu ya wakimbizi wa ndani kutokana na vita vya muda mrefu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter