Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umetangaza jopo la uchunguzi dhidi ya tukio la flotila Gaza la mwezi Mai

UM umetangaza jopo la uchunguzi dhidi ya tukio la flotila Gaza la mwezi Mai

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametangaza jopo la wataalamu wa kuchunguza tukio la flotilla lililotokea Gaza mwezi mai.

Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita Katibu Mkuu amekuwa akijihusisha na mazungumzo na mashauriano na viongozi wa Israel na Uturuki kuhusu tukio la flotilla. Jopo hilo litaongozwa na Sir Geofrey Palmer waziri mkuu wa zamani wa New Zealand kama mwenyekiti, na Rais wa Colombia anayeondoka madarakani Alvaro Uribe kama makamu mwenyekiti. Pia amesema watu wengine wawili wataongezwa kutoka Israel na Uturuki. Akitangaza jopo hilo Ban amesema ana imani litasaidia kutegua kitendawili cha nini hasa kilitokea.

(SAUTI BAN KI-MOON)

Jopo hilo linatarajiwa kuanza kazi Agosti 10 na kuwasilisha ripoti ya kwanza ya maendeleo kwa Katibu mkuu katikati ya September. Ban amesema ana matumaini kwamba kuanzishwa kwa jopo hilo kutasaidia kuimarisha uhusiano baina ya Israel na Uturuki na kuchangia pakubwa katika amani ya mashariki ya kati.