Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yanatoa msaada kwa waathirika wa mafuriko Afghanistan

Mashirika ya UM yanatoa msaada kwa waathirika wa mafuriko Afghanistan

Mashirika ya misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yanatoa msaada kwa wakazi wa mshariki mwa Afghanistan walioathirika na mafuriko.

Mafuriko hayo yaliyoshika kasi wiki hii, yameshakatili maisha ya mtu mmoja na uharibifu mkubwa wa nyumba na miundombinu. Kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na shirika la mpango wa chakula duniani WFP wameungana na mashirika yasiyo ya kiserikali na uongozi wa eneo hilo kugawa misaada katika miji na vijiji vilivyoathirika.

Miongoni mwa misaada wanayopewa ni mahema, vyandarua, mablanketi, ndoo za kumwagilia na vyombo vya jikoni. WFP kwa upande wake imeahidi kugawa chakula kitakachotosheleza kwa miaezi mitayu ijayo kwa waathirika. Majimbo manne yameathirika na mafuriko hayo , Nangarha, Laghman, Kunar na Nuristan, lakini jimbo la Nangarhar ndilo lililoathirika zaidi na hasa mji mkuu wake Jalalabad.