Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lishe bora inaweza kuimarisha matibabu kwa watu wanaoishi na virusi vya HIV:WFP

Lishe bora inaweza kuimarisha matibabu kwa watu wanaoishi na virusi vya HIV:WFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP linawataka wahudumu wa afya, serikali na wadau wengine kuongeza kionjo kingine kwenye matibabu ya watu wanaoishi na virusi vya IHV, nacho ni lishe bora.

Mkuu wa kitengo cha lishe na HIV wa shirika hilo Martin Bloem anasema kuna ongezeko la ushahidi kwamba chakula na msaada wa lishe ni muhimu kwa kuwaweka na afya njema kwa muda mrefu watu wanaoishi na virusi vya HIV na pia inasaidia matibabu kufanya kazi vizuri.

Bloem akizungumza kwenye mkutano wa ukimwi mjini Vienna, ameongeza kuwa kama watu hawawezi kupata chakula ni vigumu kutumia dawa za kurefusha maisha na hatari ya wengi kuziacha kabisa inaongezeka.