Skip to main content

ILO imezindua viwango vipya vya kazi kwenye mkutano wa UNAIDS

ILO imezindua viwango vipya vya kazi kwenye mkutano wa UNAIDS

Shirika la kazi duniani ILO limezindua mfululizo wa matukio chini ya kauli mbiu ‘kuzuia HIV, kulinda haki za binadamu kazini\'.

Ufunguzi huo umefanyika katika mkutano wa ukimwi wa 2010 ili kuadhimisha uzinduzi wa mapendekezo mapya.

ILO itajikita katika kuanzisha ushirikiano wenye nguvu na wahisani wa jumuiya ya kimataifa, watekelezaji wa masuala ya HIV na watu wanaoishi na virusi vya HIV, ili kupunguza unyanyapaa na ubaguzi kwa wafanyakazi wote wanaoishi na HIV au wanaoaminika kuwa na virusi hivyo na kuweza kuwapa nguvu mpya ya juhudi za kuzuia hali hiyo.