Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID imearifu kuzuka mapigano mapya eneo la Darfur Sudan

UNAMID imearifu kuzuka mapigano mapya eneo la Darfur Sudan

Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kwenye jimbo la Darfur Sudan UNAMID, umearifu kuzuka kwa mapigano mapya kwenye jimbo hilo.

Kwa mujibu wa UNAMID siku ya Jumanne wiki hii jeshi la serikali ya Sudan lilipambana vikali na wapiganaji wa kundi la Justice and Equality Movement JEM karibu na mlima Adola na mji wa Kuma Kaskazini mwa Darfur. Idadi kamili ya waliokufa katika vita hivyo haijafahamika na UNAMID pia inachunguza taarifa za kuzuka mapigano mengine kama hayo katika mji wa Daba Tago hukohuko kaskazini mwa Darfur

Wakati huohuo msemaji mwandamizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema UNAMID inaendelea kukabiliana na vikwazo katika shughuli zake.

(SAUTI YA FARHAN HAQ)

Haq amesema makundi hayo ya misaada hayawezi kusafiri kwa kutumia barabara kutokana na sababu za kiusalama na barabara nyingi kuharibiwa kutokana na mvua zinazonyesha.