Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matatizo yanayoikumba dunia hivi sasa yanaonyesha haja ya kuchagiza usalama:Ban

Matatizo yanayoikumba dunia hivi sasa yanaonyesha haja ya kuchagiza usalama:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisitiza haja ya kuchagiza usalama wa watu kwa kuzingatia kwamba changamoto zinazoikabili dunia hivi sasa zinatishia maisha ya mamilioni na kurudisha nyuma juhudi za maendeleo.

Ban amesema kila mtu ana haki ya kufurahia uhuru bila woga, bila mahitaji, na uhuru wa kuishi kwa heshma. Ban ameyasema hayo kwa njia ya video kwa washiriki wa kongamano la usalama wa watu linalofanyika mjini Tokyo.

Ameongeza kuwa wakati huu kuliko mwingine wowote tunaishi katika dunia iliyoungana, ambapo matatizo yanavuka mpaka na kutishia maisha ya mamilioni ya watu, wanawake, wanaume na watoto, na hiyo kuongeza hofu na kutishia kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ifikapo 2015.

Amesema kongamano hilo linaweza kusaidia kuarifu na kujadiliana zaidi kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa Septemba mjini New York utakaojikita katika malengo ya milenia.