Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati sasa ni wa Asia kuchukua jukumu katika uchumi wa kimataifa:IMF

Wakati sasa ni wa Asia kuchukua jukumu katika uchumi wa kimataifa:IMF

Asia imechipuka na kuwa imara katika uchumi wa kimataifa baada ya mdodroro wa uchumi ulioikumba dunia hivi karibuni.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa shirika la fedha duniani IMF Dominique Strauss-Kahn akihutubia mkutano wa 21 wa ngazi ya juu barani Asia mjini Daejeon Korea. Kahn amesema wakati wa Asia umefika , na hakuna atakayekuwa na mashaka kwamba umuhimu wa uchumi wa Asia utaendelea kukuwa .

Ameongeza kuwa kwa mtazamo wake mabadiliko ya kiuchumi, masuala ya fedha na sekta ya ushirika yaliyowekwa katika muongo uliopita yamechangia pakubwa katika bara hilo. Hivyo licha ya kuathirika vibaya hapo awali, Asia imeweza kujikakamua na kurejea haraka katika uchumi kutoka kwenye mdororo.