Skip to main content

Hatari, msaada na fursa vinaathiri maisha ya watoto Haiti:UNICEF

Hatari, msaada na fursa vinaathiri maisha ya watoto Haiti:UNICEF

Wakati huohuo changamoto za kufikia mahitaji ya watoto zaidi ya laki nane walioathirika na familia zao, bado ni kubwa miezi sita baada ya tetemeko kubwa kuwahi kukikumba kisiwa cha Haiti katika miaka 200.

Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Athony Lake anasema tetemeko la ardhi lililokumba Haiti lilikuwa ni janga kubwa kwa watoto na athari zake hazijamalizika bado.

Ameongeza kuwa UNICEF na washirika wake wanafanya kazi kwa bidii kila siku ili kuokoa maisha na kusaidia watoto wa nchi hiyo kuweza kupata tena hatma ya maisha yao.