Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya hatua zilizopigwa baada ya tetemeko bado kuna changamoto Haiti:UM

Licha ya hatua zilizopigwa baada ya tetemeko bado kuna changamoto Haiti:UM

Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yanasema miezi sita baada ya tetemeko la ardhi lililokatili maisha ya watu 200,000 Haiti bado kuna changamoto kubwa.

Mashirika hayo yanayohusika na kutaribu na kutoa misaada ya afya, kuhudumia watoto, haki za binadamu, masuala ya wakimbizi, uhamiaji na mazingira, yakizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva leo yamesema ingawa athari kubwa za tetemeko hilo zimeepukwa lakini bado kuna changamoto ili kuhakikisha maisha ya watu yanarejea katika hali ya kawaida.

Yamesema watu milioni moja na nusu sasa wana malazi ya dharura, milioni nne wamepata msaada wa chakula,zaidi ya milioni moja wanapata maji safi ya kunywa na asilimia 80 ya watu mjini Port-au-Prince wanapapata huduma za afya. Paul Garwood ni kutoka WHO

(SAUTI YA PAUL GARWOOD)