Skip to main content

Naomi Campbell atakiwa kutoa ushahidi katika kesi ya Charles Taylor

Naomi Campbell atakiwa kutoa ushahidi katika kesi ya Charles Taylor

Mwanamitindo mashuhuri Duniani Naomi Campbell, ametakiwa kutoa ushahidi katika mahakama ya Kimataifa ya The Hegue, katika kesi inayoendelea ya kiongozi wa zamani wa Liberia Charles Taylor.

Haiti ya kumtaka mwanamitindo huyo kutoa ushahidi imetolewa na anatakiwa kutoa ushahidi huo Julai 29 mwaka huu, katika mahakama maalum ya vita vya Sierra Leone. Vyombo mbalimbali vya habari vimesema mahakama inataka kumhoji Campbell, ukweli kuhusu tuhuma za yeye kupatiwa Almasi iliyochimbwa vitani na kuuzwa kwa ajili vya kufadhili vita hivyo, wakati kiongozi huyo alipohudhuria chakula cha jioni kwa Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela mwaka 1997.