Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kuongeza mara mbili idadi ya watu wanaopokea msaada wa chakula Niger

WFP kuongeza mara mbili idadi ya watu wanaopokea msaada wa chakula Niger

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limetangaza kuwa linaongeza shughuli zake katika nchi ya Niger inayokumbwa na ukame. WFP inasema imeamua kufanya hivyo baada ya matokeo ya utafiti wa serikali kuonyesha kwamba kiwango cha utapia mlo miongoni mwa watoto ni cha kutisha.

Ripoti ya mwaka ya serikali kuhusu lishe ya watoto inaonyesha kwamba kiwango cha kimataifa cha utapia mlo nchini humo kimefikia asilimia 16.7 kwa watoto wa chini ya umri wa miaka mitano ikilinganishwa na asilimia 12.3 ya mwaka 2009.

Shirika la afya duniani WHO linachukulia kiwango chochote kinachozidi asilimia 15 kuwa ni cha dharura. Emilia Casella ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA CASELLA)