Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malawi imeshinda tenda ya kuliuzia chakula Shirika la mpango wa chakula duniani WFP

Malawi imeshinda tenda ya kuliuzia chakula Shirika la mpango wa chakula duniani WFP

Kwa mara ya kwanza shirika la wakulima nchini Malawi lenye jumla ya wakulima wadogowadogo 95,000 wiki hii limeshinda tenda ya kuliuzia chakula shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

Mraddi wa P4P hivi sasa umezinduliwa kama wa majaribio katika nchi 21 ikiwemo Malawi na ununuzi wa tani hizo 50 za chakula umefanywa kupitia kitengo cha ubadilishanaji wa bidhaa za kilimo kwa Afrika ACE kilichoko mjini Lilongwe.

Mradi wa P4P unafadhiliwa na Bill na Melinda Gates, tume ya Ulaya, mfuko wa Howard G Buffett, serikali za Ubeligiji, Canada, Ireland, Lexembourg, Marekani na ufalme wa Saudia.