Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Kisomali wanakabiliwa na hatari na vikwazo wanapokimbilia kwenye usalama:UNHCR

Wakimbizi wa Kisomali wanakabiliwa na hatari na vikwazo wanapokimbilia kwenye usalama:UNHCR

Nchini Somalia licha ya kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama na mazingira ya kibinadamu, takwimu za karibuni zinaonyesha idadi ya wakimbizi wanaokimbilia nchi jirani imepungua.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema idadi hiyo imepungua sana ukilinganisha na mwaka jana katika kipindi kama hiki. Idadi ya waakimbizi wa Kisomali waliowasili Yemen na Kenya nchi ambazo kwa jadi zinakuwa na wakimbizi wengi wa Kisomali imepunguza sana.

UNHCR inasema sababu kubwa ni kwamba hakuna usalama na mazingira ya kuridhisha na hali inazidi kuwa mbaya.

(SAUTI YA EDWARDS)