Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango mpya wa UM nchini DR Congo MUNUSCO umeanza rasmi leo

Mpango mpya wa UM nchini DR Congo MUNUSCO umeanza rasmi leo

Mpango mpya wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MUNUSCO leo tarehe mosi Julai ndio unaanza kazi rasmi kuchumua nafasi ya MONUC.

Katika hafla maalumu ya kuzindua mpango , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema MUNUSCO itajikita zaidi katika masuala ya kusaidia kuirejesha Congo katika hali ya utulivu na kuhakikisha amani ya kudumua. Ban ameongeza kuwa hilo ni jukumu la Umoja wa Mataifa kwa nchi hiyo ambayo imesambaratishwa na vita kwa muda mrefu, pia ni jukumu lake kwa ukanda mzima na jumuiya ya kimataifa.

Amesema Umoja wa Mataifa utafanya kazi bega kwa began a serikali ya Congo ili kuwaongoza katika mchakato wa kuondoa vikosi vya kulinda amani nchini humo kwa njia ambayo haitoathiri hatua iliyopigwa na nchi hiyo Amesisitiza kwamba ni lazima kuendelea kuhakikisha kwamba wanatoa kipaumbele katika kuwalinda raia hususan wanawake ambao daiama hubeba mzigo mkubwa.