Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hospitali ya Keysaney Somalia imeendelea kushambuliwa kwa maguruneti

Hospitali ya Keysaney Somalia imeendelea kushambuliwa kwa maguruneti

Pamoja na kuzitaka pande zinazopigana kuheshimu maeneo ya Hospitali, mashambulizi yame endelea kwa siku ya tatu sasa karibu na Hospitali ya Keysaney Mashariki mwa Mogadishu nchini Somalia.

Mkuu wa ujumbe wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, Pascal Mauchle ameshangazwa na kushtushwa na pande zinazopigana kutoheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu. Sheria hiyo inataka maeneo kama ya Hospitali kuheshimiwa na kutoshambuliwa wakati wa vita.

Kwa mara nyingine tena,kamati hiyo imesihi pande zinazo pigana kutofanya mashambulizi kwenye taasisi za Afya. Mpaka sasa Hospitali ya Keysaney imeshahudumia wagonjwa 1,400 bila kujali tabaka, wakiwemo Wanawake 300 na watoto 200.