Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lazima lizingatie utawala wa sheria asema Migiro

Baraza la usalama lazima lizingatie utawala wa sheria asema Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro amesema katika wakati huu ambao dunia inakabiliwa na vitisho vya amani na usalama wa kimataifa lazima baraza la usalama lizingatie utawala wa sheria linapochukua hatua.

Bi migiro aliyezungumza hayo kwenye mjadala wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu utawala wa sheria, amesema mambo kama uhalifu wa kupangwa, ugaidi na uharmia yanatishia amani ya dunia.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kwamba kwama njia ya kuzuia,  Umoja wa Mataifa lazima ulipe kipumbele suala la usalama, uwezekano wa haki na ulindwa kisheria kwa wote na kuhakikisha kwamba inakuwa rahisi kwa migogoro katika jamii kutatatuliwa kwa njia ya kisheria badala ya kutumia nguvu.

Lakini wakati huohuo amesema katika kukabiliana na uhalifu wa kimataifa Umoja wa Mataifa lazima uzidishe mara mbili juhudi zake za kutoa uwezo wa kitaifa kuwakamata washukiwa wa uhalifu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.