Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ECOSOC imeanza mjadala wa pili kuhusu ushirikiano na maendeleo

ECOSOC imeanza mjadala wa pili kuhusu ushirikiano na maendeleo

Baraza la jamii na uchumi leo limeanza majadilino ya pili ya maendeleo na ushirikiano, ambayo yanajikita katika mijadala ya wadau mbalimbali wakigusia masuala ya ushirikiano wa kimataifa wa maendeleo ,ugawaji wa miasaada, utekelezaji na muingiliano wa sera.

Rais wa ECOSOC Hamodon Ali akizungumza katika ufunguzi wa majadiliano hayo yaliyoanzishwa na mkutano wa dunia wa mwaka 2005 amesema, yanatoa fursa ambayo hatuwezi kuikosa ya kutoa mapendekezo muhimu ya kuelekea kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia kwa misingi ya ushirikianomzuri zaidi wa maendeleo.

Ameongeza kuwa kwa kuzingatia mabadiliko ya uchumi wa dunia na misaada ya kihandisi, jukumu la misaada rasmi ya maendeleo ODA na misaada mingine ya kifedha ya maendeleo ni muhimu sana kuhakikisha hatua zinapigwa katika kuelekea kutimiza malengo hayo sasa kuliko wakati mwingine wowote.