Je nchi za Afrika zitaweza kufikia malengo ya maendeleo ya milenia?

25 Juni 2010

Mjini Mombasa Kenya Ijumaa hii kumemalizika kongamano la kimataifa la uongozi, usimamizi na utawala bora likijumuisha washiriki kutoka sehemu mbalimbali.

Kongamano hilo limeandaliwa na serikali ya Kenya ambaye amekuwa mwenyeji kwa ufadhili mkubwa wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP. Kongamano hilo limejadili miaka 10 kuanzia sasa afrika itakuwa imepiga hatua kiasi gani katika kufanikisha mahitaji ya watu wake, kisiasa, kiuchumi na kijamii. Je malengo ya maendeleo ya milenia yatafikiwa?

Kutana na mchambuzi, wakili na msimamizi wa kongamano hilo profesa Patrice Lumumba akizungumza na mwandishi Radio ya Umoja wa Mataifa Irene Mwakesi.

l

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter