Skip to main content

WFP imeingiza misaada zaidi kuwasaidia wakimbizi wa Kyrgystan

WFP imeingiza misaada zaidi kuwasaidia wakimbizi wa Kyrgystan

Juhudi za kufikisha msaada Kyrygystan zimetiwa nguvu hii leo na shirika la mpango wa chakula WFP baada ya kuwasili na ndege iliyosheheni msaada mjini Osh.

Msaada huo wa dharura ni pamoja na chakula n a biskuti kwa watu 30,000 ambao wameathirika na machafuko ya karibuni, makoti ya kujikinga na risasi  pamoja na vifaa vya mawasiliano ili kusaidia usambazaji wa misaada ya kibinadamu.

Wakati huohuo WFP imefungua kituo mjini Osh ili kuwa kama kiungo cha kupokea misaada kutoka jumuiya zote zinazotoa msaada nchini humo.Tangu kuzuka kwa machafuko WFP imeshawasaidia kwa chakula watu 54,000 mjini Osh na Jalalabad na imetoa wito wa msaada wa dola milioni 19 ili kuendelea kugawa chakula kwa wahitaji.