Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi zaidi zinahitajika kuwasaidia wakimbizi wa ndani na nje:UNHCR

Juhudi zaidi zinahitajika kuwasaidia wakimbizi wa ndani na nje:UNHCR

Wakati dunia imeadhimisha siku ya wakimbizi jana Jumapili, Kamishina Mkuu wa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Antonio Guterres ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza juhudi kuwasaidia wakimbizi.

Bwana Guterres ametoa wito huo nchini Syria kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kukutana na Rais wa nchi hiyo Bashar Assad. Syria inahifadhi wakimbizi milioni moja wa Iraq.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon pia ametoa wito kwa niaba ya wakimbizi akisema, wakimbizi wamepokonywa nyumba zao lakini wasipokonywe hatma ya maisha yao. Mmoja wa wakimbizi wa Kisomali anayeishi Kenya ni Anna Busheikh anatamani hali ingetengemaa arejee nyumbani.

(SAUTI YA ANNA BUSHEIKH KENYA)