Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya kufuatilia uchunguzi wa Israel na Palestina dhidi ya flotila yatajwa

Kamati ya kufuatilia uchunguzi wa Israel na Palestina dhidi ya flotila yatajwa

Kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay ametangaza kamati ya wataalamu watatu wa kujitegemea kufuatilia uchunguzi wa Israel na Palestina kuhusu shambulio la flotilla.

Wataalamu hao wanapewa jukumu na baraza la haki za binadamu kufuatilia uchunguzi dhidi ya ukiukwaji wa masuala ya kibinadamu na haki za binadamu za kimataifa ulioarifiwa na mpango wa Umoja wa Mataifa wa uchunguzi ulioongozwa na Richard Goldstone. Wataalamu hao ni Profesa Christian Tomuschat wa Ujerumani ambaye pia ni mwenyekiti wa tume, Jaji Mary McGowan Davis wa Marekani na bwana Param Cumaraswamy wa Malaysia.

Kamati hiyo chini ya jukumu la mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa itafuatilia na kuopima uchuguzi wowote utakaofanyika kinyumbani au kisheria na serikali za Israel na Palestina ikiwa ni pamoja na uchunguzi binafsi, uhalali wake, ukweli wake na kuzingatia kwakwe viwango vya kimataifa.