Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amekaribisha makubaliano ya Eritrea na Djibout kuhusu mzozo wa mpaka

Ban amekaribisha makubaliano ya Eritrea na Djibout kuhusu mzozo wa mpaka

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekaribisha hatua ya Eritrea na Djibout kutia saini makubaliano ya kutatua mzozo wao wa mpaka chini ya upatanishi wa serikali ya Qatar.

Mzozo wa mpaka baina ya nchi hizo mbili ulizuka Machi 2008. Katibu Mkuu ametoa shukrani zake kwa serikali ya Qatar kufanikisha ushuluhishi huo. Makubaliano hayo yameipa jukumu Qatar kuanzisha njia ya suhuhu ya mzozo huo na kurejesha uhusiano baiana ya nchi hizo mbili.

Katibu Mkuu amesema ametiwa shime na hatua hiyo ya matumaini ambayo anaamini itachangia amani ya muda mrefu na utulivu katika pembe ya Afrika.