Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanadiplomasia wa Tanzania kuuwakilisha Umoja wa Mataifa Somalia

Mwanadiplomasia wa Tanzania kuuwakilisha Umoja wa Mataifa Somalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa leo amemteua mwanadiplomasia wa Tanzania kumwakilisha nchini Somalia.

Mwanadiplomasia huyo Augustin Mahiga ni balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa na ana uzoefu mkubwa wa kufanya kazi katika maeneo yenye migogoro hususani upatanishi na mipango ya amani. Mahiga amekuwa akishughulika na masuala ya maendeleo, amani na usalama, haki za binadamu na kuimarisha uhusiano baina ya Umoja wa Afrika ya Umoja wa Mataifa.

Balozi Mahiga atachukua nafasi ya Ahmedou Ould-Abdallah wa Mauritania.

Somalia inamatatizo mengi ya kiusalama huku wanamgambo wakitishia kuiangusha serikali ya mpito inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, na pia inakabiliwa na tatizo la uharamia.