Ban Ki-moon akutana na serikali Burundi na wafanyakazi wa UM

Ban Ki-moon akutana na serikali Burundi na wafanyakazi wa UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon yuko nchini Burundi kwa ziara ya siku moja. Ban alipowasili tuu amesema huu ni mwaka mzuri kwa Afrika mbali ya kuandaa mashindano ya kombe la dunia pi nchi kama Burundi ni ya kupongezwa kwa juhudi iliyopiga kutafuta amani ya nchi hiyo.

Pia amesifu mchango mkubwa wa Burundi kusaidia kutafuta amani nchini Somalia kwa kuchangia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika. Katika muda huo mfupi Ban amekutana na viongozi wa serikali, bunge, viongozi wa vyama vya siasa, tume ya uchaguzi , jumuiya za kiraia na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa. Akizungumza bungeni leo Ban amesema pamoja na kwamba nchi hiyo imepiga hatua lakini bado kuna changamoto