Skip to main content

Mkuu wa WHO ateta kuhusu madai kuwa lilichagizwa na mashirika ya dawa kuhusu homa ya H1N1

Mkuu wa WHO ateta kuhusu madai kuwa lilichagizwa na mashirika ya dawa kuhusu homa ya H1N1

Mkuu wa Shirika la Afya duniani, WHO leo ameongea dhidi ya shutma kwamba shirika hilo lilishirikiana na makampuni ya kutengeneza madawa katika kupamabana na homa ya mafua ya H1N1.

Taarifa kwenye jarida la kitabibu la Uingereza inasema WHO ilipata mawaidha kutoka kwa wataalamu ambao pia walikuwa wanalipwa na makampuni ya kutengeneza madawa kuhusu juhudi za kupambana na homa hiyo.

Mkurugenzi wa WHO Bi Margaret Chan amesema kuwa katika uhusiano baina ya makampuni ya kutengeneza madawa ambayo lengo lao ni kutafuta faida na shirika lisilotafuta faida kama Umoja wa Mataifa lazima kutakuwepo na tofauti za kimtazamo.

Ameongeza kuwa WHO ilifuata misingi ya kimataifa ya afya katika kukabiliana na ugonjwa unapolipuka na halikupata shinikizo wala ushawishi kutoka kwa kampuni yoyote.