Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kaka na WFP wazindua mafunzo kwa vijana ya kupambana na njaa

Kaka na WFP wazindua mafunzo kwa vijana ya kupambana na njaa

Wakati huohuo mashindano ya kombe la dunia yakikaribia balozi mwema wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP ambaye pia ni mwanakandanda bora wa dunia Kaka wamezindua mafunzo maalumu kwa vijana.

Mafunzo hayo ni kuwaelimisha vbijana umuhimu wa kupambana na njaa na mbinu bora za kuwasaidia watu bilioni moja duniani wawe na chakula cha kutosha.

Kwa mujibu wa Kaka njia moja ya kupambana na njaa ni kuhakikisha kwamba karibu watoto milioni 66 ambao hawana chakula wanapata chakula kila siku shuleni.